Publicidade

Sonhos

Por Bíblia Online

Sonhos aparecem em toda a Bíblia como meio de revelação divina. Deus falou através de sonhos a patriarcas, profetas e servos, mas também alertou contra falsos sonhadores.

Sonhos como revelação divina

Deus usou sonhos para comunicar sua vontade a homens e mulheres ao longo da história bíblica, revelando caminhos e mistérios.

Bwana akasema, "Sikilizeni maneno yangu:

"Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,

nitajifunua kwake kwa maono,

nitanena naye katika ndoto.

Siku Ya Bwana

"Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

Petro Ahutubia Umati

Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akainua sauti yake na kuhutubia ule umati wa watu, akasema: "Wayahudi wenzangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, jueni jambo hili mkanisikilize. Hakika watu hawa hawakulewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:

" Katika siku za mwisho, asema Mungu,

nitamimina Roho wangu

juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

vijana wenu wataona maono,

na wazee wenu wataota ndoto.

Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.

Mfalme akamuuliza Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza), "Je, unaweza kuniambia nilichoona katika ndoto yangu na kuifasiri?"

Danieli akajibu, "Hakuna mwenye hekima, msihiri, mganga au mwaguzi anayeweza kumweleza mfalme siri aliyouliza, lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:

Sonhos na história da Bíblia

De José no Egito a José pai de Jesus, Deus guiou a história da salvação através de sonhos, protegendo e dirigindo seu povo.

Wakamjibu, "Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri."

Ndipo Yosefu akawaambia, "Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu."

Farao akamwambia Yosefu, "Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia ikisemwa kwa habari yako kwamba unapoelezwa ndoto waweza kuifasiri."

Yosefu akamjibu Farao, "Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji."

Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, "Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu, kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu. kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao."

Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: "Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."

Kurejezwa Kutoka Utumwani
Wimbo wa kwenda juu.

Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,

tulikuwa kama watu walioota ndoto.

Sabedoria sobre sonhos

A Bíblia ensina discernimento: nem todo sonho vem de Deus. Devemos entregar nossos planos ao Senhor e confiar na direção dele.

Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo,

nayo mipango yako itafanikiwa.

Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,

lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

Kuabudu Miungu Mingine

Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, "Na tufuate miungu mingine" (miungu ambayo hamjaifahamu) "na tuiabudu," kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. Bwana Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote. Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.

"Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe?

Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo," asema Bwana. "Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo," asema Bwana.

Kama vile ndoto huja

wakati kuna shughuli nyingi,

ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu

wakati kuna maneno mengi.

Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo simama katika kicho cha Mungu.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-