Temor do Senhor
O temor do Senhor é o princípio da sabedoria. Não se trata de medo, mas de reverência profunda, respeito e admiração diante da santidade e grandeza de Deus.
O princípio da sabedoria
A Escritura afirma que temer ao Senhor é o primeiro passo para a verdadeira sabedoria. Quem teme a Deus discerne o certo e aprende a viver com prudência.
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.
"Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima,
nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.
Naye Mungu akamwambia mwanadamu,
‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,
nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ "
Kumcha Bwana ni utakatifu,
nako kwadumu milele.
Amri za Bwana ni za hakika,
nazo zina haki.
Ni za thamani kuliko dhahabu,
kuliko dhahabu iliyo safi sana,
ni tamu kuliko asali,
kuliko asali kutoka kwenye sega.
Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,
katika kuzishika kuna thawabu kubwa.
Bênçãos do temor
Quem teme ao Senhor encontra vida longa, provisão e proteção. O temor de Deus nos guarda do mal e nos conduz à humildade.
Unyenyekevu na kumcha Bwana
huleta utajiri, heshima na uzima.
Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha,
lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;
kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.
Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,
bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu
huangukia kwenye taabu.
Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
Mcheni Bwana enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.
Vivendo no temor do Senhor
Temer ao Senhor é obedecer seus mandamentos, andar em seus caminhos e amá-lo de todo coração. Essa reverência se expressa em justiça e integridade.
Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Shikeni maagizo ya Bwana Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu.
Mtumikieni Bwana kwa hofu
na mshangilie kwa kutetemeka.
Njooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.
Yeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
basi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
Aache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.
Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa."
" ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
" ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako. Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi katikati yako.
"Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!