Publicidade

Temor do Senhor

Por Bíblia Online

O temor do Senhor é o princípio da sabedoria. Não se trata de medo, mas de reverência profunda, respeito e admiração diante da santidade e grandeza de Deus.

O princípio da sabedoria

A Escritura afirma que temer ao Senhor é o primeiro passo para a verdadeira sabedoria. Quem teme a Deus discerne o certo e aprende a viver com prudência.

Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,

Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri,

Sifa zake zadumu milele.

Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;

Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima;

Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Kisha akamwambia mwanadamu,

Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima,

Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Kicho cha BWANA ni kitakatifu,

Kinadumu milele.

Hukumu za BWANA ni kweli,

Zina haki kabisa.

Ni za kutamanika kuliko dhahabu,

Kuliko wingi wa dhahabu safi.

Nazo ni tamu kuliko asali,

Kuliko sega la asali.

Tena mtumishi wako huonywa kwazo,

Katika kuzishika kuna thawabu kuu.

Bênçãos do temor

Quem teme ao Senhor encontra vida longa, provisão e proteção. O temor de Deus nos guarda do mal e nos conduz à humildade.

Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA

Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.

Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu;

Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.

Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima,

Ili kuepukana na tanzi za mauti.

Kwa rehema na kweli uovu husafishwa;

Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.

Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote;

Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.

Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema;

Heri mtu yule anayemtumainia.

Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,

Maana, wamchao hawapungukiwi kitu.

Vivendo no temor do Senhor

Temer ao Senhor é obedecer seus mandamentos, andar em seus caminhos e amá-lo de todo coração. Essa reverência se expressa em justiça e integridade.

Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

Nawe uzishike amri za BWANA, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha.

Mtumikieni BWANA kwa kicho,

Shangilieni kwa kutetemeka.

Njoni, enyi wana, mnisikilize,

Nami nitawafundisha kumcha BWANA.

Ni nani atamaniye uzima na atakaye kuishi,

Siku nyingi afurahie mema?

Uuzuie ulimi wako na mabaya,

Na midomo yako na kusema hila.

Uache mabaya ukatende mema,

Utafute amani ukaifuatie.

Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.

Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.

Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.

Mahimizo ya kukiri bila woga

Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanamu; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-