Publicidade

Vaso

Por Bíblia Online

A metáfora do vaso é uma das mais belas da Bíblia. Assim como o oleiro molda o barro, Deus nos forma segundo seus propósitos, fazendo de nós vasos úteis para sua glória.

Nas mãos do oleiro

Deus é o Oleiro e nós somos o barro. Ele tem autoridade e sabedoria para nos moldar conforme sua vontade perfeita, e não devemos questionar sua obra.

Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu.

Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi;

sisi sote tu kazi ya mkono wako.

Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: "Shuka uende mpaka nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu." Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kama vile ilivyoonekana vyema kwake yeye.

Kisha neno la Bwana likanijia kusema: "Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?" asema Bwana. "Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli.

Lakini, ewe mwanadamu, u nani wewe ushindane na Mungu? "Je, kilichoumbwa chaweza kumwambia yeye aliyekiumba, ‘Kwa nini umeniumba hivi?’ " Je, mfinyanzi hana haki ya kufinyanga kutoka bonge moja vyombo vya udongo, vingine kwa matumizi ya heshima na vingine kwa matumizi ya kawaida?

"Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,

yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.

Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,

‘Unatengeneza nini wewe?’

Je, kazi yako husema,

‘Hana mikono’?

Mnapindua mambo juu chini,

kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!

Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,

"Wewe hukunifinyanga mimi?"

Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,

"Wewe hujui chochote?"

Vasos para honra

O cristão é chamado a ser um vaso de honra, purificado e preparado para toda boa obra. Nosso valor está em quem nos formou e no que carregamos.

Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida. Basi ikiwa mtu amejitakasa na kujitenga na hayo niliyoyataja, atakuwa chombo maalum, kilichotengwa na ambacho kinamfaa mwenye nyumba, kimeandaliwa tayari kwa kila kazi njema.

Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu.

Wana wa Sayuni wenye thamani,

ambao mwanzo uzito wa thamani yao

ulikuwa wa dhahabu,

sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo,

kazi ya mikono ya mfinyanzi!

Moldados pela graça

Mesmo quando nos sentimos frágeis e imperfeitos, o poder de Deus se aperfeiçoa em nossa fraqueza. Ele nos restaura e nos renova continuamente.

"Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.

Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.

Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?

Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo

ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.

Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,

mgaagae mavumbini,

ninyi viongozi wa kundi.

Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;

mtaanguka na kuvunjavunjwa

kama vyombo vizuri vya udongo.

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-22_10-02-25-