Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wakorintho 1:10-12

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa

10 Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. 11 Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, "Mimi ni wa Paulo"; mwingine, "Mimi ni wa Apolo"; mwingine, "Mimi ni wa Kefa,"1:12 Yaani Petro. na mwingine, "Mimi ni wa Kristo."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    10 Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano kati yenu, na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. 11 Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi kati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, "Mimi ni wa Paulo"; mwingine, "Mimi ni wa Apolo"; mwingine, "Mimi ni wa Kefa1:12 yaani Petro"; na mwingine, "Mimi ni wa Al-Masihi."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    10 Flp 2:2;3:16Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu migawanyiko, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba uko ugomvi kwenu. 12 Mdo 18:24,27;1 Kor 3:4;Yn 1:42Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.