Karama Za Rohoni
1 Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 3 Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, "Yesu na alaaniwe." Pia hakuna mtu awezaye kusema, "Yesu ni Bwana," isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.
4 Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.
7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.