Karama Za Unabii Na Lugha
1 Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii. 3 Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji.
24 Lakini kama mtu asiyeamini au asiyeelewa akiingia wakati kila mtu anatoa unabii, ataaminishwa na watu wote kuwa yeye ni mwenye dhambi na kuhukumiwa na wote, 25 nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, "Kweli Mungu yuko katikati yenu!"
29 Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo. 30 Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze. 32 Roho za manabii huwatii manabii.