Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wakorintho 14:26-29,33,40

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Kumwabudu Mungu Kwa Utaratibu

26 Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kanisa. 27 Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.

29 Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani.

Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu,

40 Lakini kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    26 Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kundi la waumini. 27 Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu, si zaidi, mmoja baada ya mwingine, na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya katika kundi la waumini, na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.

    29 Manabii wawili au watatu wanene, na wengine wapime kwa makini yale yasemwayo. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani.

    Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu,

    40 Lakini kila kitu kitendeke kwa ufasaha na kwa utaratibu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    26 1 Kor 11:18;12:8;Efe 4:12Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. 27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. 28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. 29 1 The 5:21;Mdo 17:11Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.

    40 Kol 2:5Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.