Mwili Wa Ufufuo
35 Lakini mtu anaweza kuuliza, "Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?" 36 Ninyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. 37 Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine. 38 Lakini Mungu huipa mbegu umbo kama alivyokusudia mwenyewe na kila aina ya mbegu huipa umbo lake.
42 Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika, 43 unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu, 44 unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho.
Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia.