Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Mambo Ya Nyakati 29:11,12,14,15

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

11 Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,

na utukufu na enzi na uzuri,

kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

ni chako wewe.

Ee Bwana, ufalme ni wako;

umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

12 Utajiri na heshima vyatoka kwako;

wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.

Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

14 "Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. 15 Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    11 Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Mwenyezi Mungu,

    na utukufu na enzi na uzuri,

    kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

    ni chako wewe.

    Ee Mwenyezi Mungu, ufalme ni wako;

    umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

    12 Utajiri na heshima vyatoka kwako;

    wewe ndiwe unayetawala vitu vyote.

    Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

    ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

    14 "Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vinavyotoka mkononi mwako. 15 Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Dan 4:34,35;Mt 6:13;1 Tim 1:17;Ufu 5:13Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. 12 Kum 8:18;1 Sam 2:7,8;Zab 75:6;Mit 10:22;Rum 11:36;Yak 1:17Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. 14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea. 15 Mwa 47:9;Zab 39:12;Ebr 11:13;1 Pet 2:11;Ayu 14:2;Zab 90:9;102:11;144:4Kwani sisi tu wageni na wapitaji mbele zako, kama walivyokuwa baba zetu wote; siku zetu duniani ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kuishi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.