Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 18:36,37

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: "Ee Bwana, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 37 Unijibu mimi, Ee Bwana, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee Bwana, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Ilya akasogea mbele na kuomba, akisema: "Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kama ulivyoagiza. 37 Unijibu, Ee Mwenyezi Mungu! Unijibu ili watu hawa wajue kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    36 Kut 29:39;Mwa 28:13;Kut 3:6;4:5;Mt 22:32;Ebr 11:16;1 Fal 8:43;2 Fal 19:19;Zab 83:18;Hes 16:28Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 37 Yer 10:23;31:18Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.