Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 18:41-46

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

41 Eliya akamwambia Ahabu, "Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa." 42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Eliya akapanda kileleni mwa Karmeli, akasujudu na akaweka kichwa chake katikati ya magoti yake.

43 Akamwambia mtumishi wake, "Nenda ukatazame kuelekea bahari." Akaenda na kutazama.

Akasema, "Hakuna kitu chochote huko."

Mara saba Eliya akasema, "Nenda tena."

44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, "Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini."

Hivyo Eliya akasema, "Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ "

45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli. 46 Nguvu za Bwana zikamjia Eliya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi maingilio ya Yezreeli.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    41 Ilya akamwambia Ahabu, "Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa." 42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Ilya akapanda kileleni mwa Karmeli, akainama hadi chini, na kuweka kichwa chake katikati ya magoti.

    43 Akamwambia mtumishi wake, "Nenda ukatazame kuelekea bahari." Akaenda na kutazama.

    Akasema, "Hakuna kitu chochote huko."

    Mara saba Ilya akasema, "Nenda tena."

    44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, "Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini."

    Hivyo Ilya akasema, "Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako la vita, ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ "

    45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli. 46 Nguvu za Mwenyezi Mungu zikamjia Ilya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi ingilio la Yezreeli.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    41 Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele. 42 Yak 5:17Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini. 43 Mwa 32:20;Hab 2:3Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Nenda tena mara saba. 44 Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Nenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie. 45 Ikawa, muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli. 46 2 Fal 3:15;Eze 1:3;3:14Mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya; akajikaza viuno, akapiga mbio akatangulia Ahabu mpaka kuiingia Yezreeli.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.