Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 19:19-21

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Wito Wa Elisha

19 Hivyo Eliya akaondoka kutoka huko na kumkuta Elisha mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliongoza ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akamrushia vazi lake. 20 Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, "Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe."

Eliya akajibu, "Rudi zako, kwani nimekutendea nini?"

21 Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    19 Hivyo Ilya akaondoka huko na kumkuta Al-Yasa mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliiongoza ile jozi ya kumi na mbili. Ilya akamwendea, na kumvisha vazi lake. 20 Kisha Al-Yasa akawaacha maksai wake, akamkimbilia Ilya, akamwambia, "Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe."

    Ilya akajibu, "Rudi zako, kwani nimekufanya nini?"

    21 Basi Al-Yasa akamwacha Ilya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Ilya, akamtumikia.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    19 Basi, akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima, mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa vazi lake juu yake. 20 Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Nenda, urudi; ni nini niliyokutendea? 21 2 Sam 24:22;Mt 4:18-22;Lk 5:27,28;Kut 24:13Akarudi akiacha kumfuata, akatwaa lile jozi la ng’ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng’ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.