20 Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, "Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe."
Eliya akajibu, "Rudi zako, kwani nimekutendea nini?"
21 Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.