5 Bwana akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, "Omba lolote utakalo nikupe."
9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu ili kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana, ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi hivi?"
10 Bwana akapendezwa kwamba Solomoni ameliomba jambo hili. 11 Basi Mungu akamwambia, "Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki, 12 nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.
Utawala Wa Hekima
16 Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake.
25 Ndipo mfalme akatoa amri: "Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu."
27 Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: "Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake."
28 Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.