Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 1:10,11,15,18,20

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

10 Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 11 Naye akaweka nadhiri, akisema, "Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake."

15 Hana akajibu, "Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Bwana.

18 Hana akasema, "Mtumishi wako na apate kibali machoni pako." Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.

20 Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina lake Samweli, akasema, "Kwa kuwa nilimwomba kwa Bwana."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    10 Kwa uchungu wake mwingi Hana alimwomba Mwenyezi Mungu, akilia kwa uchungu. 11 Naye akaweka nadhiri, akisema, "Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Mwenyezi Mungu kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake."

    15 Hana akajibu, "Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Mwenyezi Mungu.

    18 Hana akasema, "Mtumishi wako na apate kibali machoni pako." Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.

    20 Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina Samweli, akisema, "Kwa kuwa nilimwomba kwa Mwenyezi Mungu."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    10 Ayu 7:11;10:1;Hes 30:3;2 Sam 17:8Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana. 11 Hes 6:5;Mwa 28:20;Hes 21:2;30:3-8;Amu 11:30;Mhu 5:4;Mwa 29:32;Kut 4:31;2 Sam 16:12;Zab 25:18;Mwa 8:1;30:22;Zab 132:1,2Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe. 15 Zab 62:8Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA. 18 Mwa 33:15;Rut 2:13;Mhu 9:7;Yn 16:24Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukuhuzunika tena. 20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; akamwita Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.