Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samuel 1

10 Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 11 Naye akaweka nadhiri, akisema, "Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake."

12 Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake. 13 Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa 14 naye akamwambia, "Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako."

15 Hana akajibu, "Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Bwana. 16 Usimdhanie mtumishi wako kuwa mwanamke mwovu; nimekuwa nikiomba hapa katika wingi wa uchungu mkuu na huzuni."

17 Eli akamjibu, "Nenda kwa amani, naye Mungu wa Israeli na akujalie kile ulichomwomba."

18 Hana akasema, "Mtumishi wako na apate kibali machoni pako." Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.

19 Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za Bwana na kisha wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye Bwana akamkumbuka. 20 Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina lake Samweli, akasema, "Kwa kuwa nilimwomba kwa Bwana."

Veja também