Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 1:5,8,11,23,27,28

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

5 Lakini alimpa Hana fungu maradufu kwa sababu alimpenda, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. 8 Elikana mumewe akawa anamwambia, "Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je, mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?"

11 Naye akaweka nadhiri, akisema, "Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake."

23 Elikana mumewe akamwambia, "Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, Bwana na akujalie kutimiza nadhiri yako." Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.

27 Niliomba mtoto huyu, naye Bwana amenijalia kile nilichomwomba. 28 Hivyo sasa ninamtoa kwa Bwana. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Bwana." Naye akamwabudu Bwana huko.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    5 Lakini alimpa Hana fungu maradufu kwa sababu alimpenda, ingawa Mwenyezi Mungu alikuwa amemfunga tumbo. 8 Elkana mumewe akawa anamwambia, "Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je, mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?"

    11 Naye akaweka nadhiri, akisema, "Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Mwenyezi Mungu kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake."

    23 Elkana mumewe akamwambia, "Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa hadi utakapomwachisha kunyonya, Mwenyezi Mungu na akujalie kutimiza nadhiri yako." Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe hadi alipomwachisha kunyonya.

    27 Niliomba mtoto huyu, naye Mwenyezi Mungu amenijalia kile nilichomwomba. 28 Hivyo sasa ninamtoa kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Mwenyezi Mungu." Naye akamwabudu Mwenyezi Mungu huko.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Mwa 30:2lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo. 8 Rut 4:15Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwa nini huli? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? 11 Hes 6:5;Mwa 28:20;Hes 21:2;30:3-8;Amu 11:30;Mhu 5:4;Mwa 29:32;Kut 4:31;2 Sam 16:12;Zab 25:18;Mwa 8:1;30:22;Zab 132:1,2Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.

    23 Hes 30:7;2 Sam 7:25Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hadi utakapomwachisha kunyonya; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hadi akamwachisha kunyonya. 27 Mt 7:7Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; 28 Mwa 24:26,52kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.