Samweli Anamtia Daudi Mafuta
1 Bwana akamwambia Samweli, "Utamlilia Sauli mpaka lini, maadamu nimemkataa asiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli? Jaza pembe yako mafuta, ushike njia uende; ninakutuma kwa Yese huko Bethlehemu. Nimemchagua mmoja wa wanawe kuwa mfalme."
6 Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, "Hakika mpakwa mafuta wa Bwana anasimama hapa mbele za Bwana."
10 Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, "Bwana hajawachagua hawa." 11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"
Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."
Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike."
12 Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.
Ndipo Bwana akasema, "Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye."
13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.