Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 16:11,12

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"

Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."

Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike."

12 Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

Ndipo Bwana akasema, "Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"

    Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."

    Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi hadi afike."

    12 Basi akatuma aitwe, naye akaletwa. Aling’aa kwa afya, na mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

    Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, "Inuka na umpake mafuta; huyu ndiye."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 1 Sam 17:12;2 Sam 7:8;Zab 78:70Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hadi atakapokuja huku. 12 Wim 5:10;1 Sam 9:17Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.