11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"
Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."
Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike."
13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.