Bwana Amwita Samweli
1 Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.
4 Kisha Bwana akamwita Samweli.
Samweli akajibu, "Mimi hapa." 5 Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, "Mimi hapa, kwa kuwa umeniita."
Lakini Eli akasema, "Sikukuita; rudi ukalale." Hivyo akaenda kulala.
6 Bwana akaita tena, "Samweli!" Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, "Mimi hapa, kwa kuwa umeniita."
Eli akasema, "Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale."
7 Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua Bwana. Neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
8 Bwana akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, "Mimi hapa, kwa kuwa umeniita."
Ndipo Eli akatambua kuwa Bwana alikuwa akimwita kijana. 9 Hivyo Eli akamwambia Samweli, "Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ " Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.
10 Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, "Samweli! Samweli!"
Kisha Samweli akasema, "Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza."