20 Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Kristo ni "Ndiyo." Kwa sababu hii ni kwake yeye tunasema "Amen" kwa utukufu wa Mungu. 21 Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Kristo. Ametutia mafuta 22 kwa kututia muhuri wake na kutupa Roho wake mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia kile kijacho.
Publicidade
Publicidade