4 Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu. 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, "Nuru na ingʼae gizani," ameifanya nuru yake ingʼae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.
2 Wakorintho 4:4-6
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
4 Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu. 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe, ila tunamhubiri Isa Al-Masihi kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Isa. 6 Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, "Nuru na ing’ae gizani," ameifanya nuru yake ing’ae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Al-Masihi.
- SRUV Swahili Revised Union Version
4 Ebr 1:3;Efe 2:2;2 The 2:11;Kol 1:15ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 5 2 Kor 1:24Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Mwa 1:3;2 Kor 3:18;Isa 9:1Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.