Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Wakorintho 6:14-18

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Msifungiwe Nira Pamoja Na Wasioamini

14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari?6:15 Beliari hapa ina maana ya uovu, kutokumcha Mungu. Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: "Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu."

17 "Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,

mkatengwe nao,

asema Bwana.

Msiguse kitu chochote kilicho najisi,

nami nitawakaribisha."

18 "Mimi nitakuwa Baba kwenu,

nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu,

asema Bwana Mwenyezi."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini. Kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna mapatano gani kati ya Al-Masihi na Beliari6:15 maana yake Uovu, yaani Shetani? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema:

    "Nitakaa pamoja nao

    na kutembea katikati yao,

    nami nitakuwa Mungu wao,

    nao watakuwa watu wangu."

    17 Kwa hiyo,

    "Tokeni miongoni mwao,

    mkatengwe nao,

    asema Mwenyezi Mungu.

    Msiguse kitu chochote kilicho najisi,

    nami nitawakaribisha."

    18 Na,

    "Mimi nitakuwa Baba kwenu,

    nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,

    asema Mwenyezi Mungu,

    Mungu wa majeshi ya mbinguni."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    14 Efe 5:11Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?6:15 Beliari: maana yake ni, Ufisadi. Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Law 26:12;Eze 37:27;1 Kor 3:16;6:19;Eze 37:27Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Isa 52:11;Yer 51:45;Eze 20:34,41;Ufu 18:4Kwa hiyo,

    Tokeni kati yao,

    Mkatengwe nao, asema Bwana,

    Msiguse kitu kilicho kichafu,

    Nami nitawakaribisha.

    18 2 Sam 7:8,14;1 Nya 17:13;Isa 43:6;Yer 31:9;32:38;Hos 1:10;Amo 4:13Nitakuwa Baba kwenu,

    Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

    asema Bwana Mwenyezi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.