Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Reis 6

Shoka Laelea

1 Wana wa manabii wakamwambia Elisha, "Tazama, mahali hapa tunapokutana nawe ni padogo sana kwetu. 2 Twendeni Yordani, mahali ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi."

Naye akawaambia, "Nendeni."

3 Kisha mmoja wao akasema, "Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?"

Elisha akajibu, "Nitakuja." 4 Naye akaenda pamoja nao.

Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. 5 Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, "Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!"

6 Mtu wa Mungu akauliza, "Je, liliangukia wapi?" Alipomwonyesha mahali penyewe, Elisha akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea. 7 Akasema, "Lichukue." Kisha yule mtu akanyoosha mkono wake, akalichukua.

Veja também