Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Samweli 5:1-7,9

Daudi Atawazwa Mfalme Juu Ya Israeli

1 Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, "Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye Bwana alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ "

3 Wazee wote wa Israeli wakamwendea Mfalme Daudi huko Hebroni, mfalme akafanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta kuwa mfalme wa Israeli.

4 Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. 5 Huko Hebroni alitawala Yuda kwa miaka saba na miezi sita, na katika Yerusalemu alitawala Israeli yote na Yuda kwa miaka thelathini na mitatu.

Daudi Ateka Yerusalemu

6 Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, "Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza." Walidhani, "Daudi hawezi kuingia humu." 7 Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

9 Ndipo Daudi akafanya makao ndani ya ngome na kuiita Mji wa Daudi. Akajenga eneo linalozunguka kuanzia Milo5:9 Milo maana yake Boma la Ngome. kuelekea ndani.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.