Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 21:15-17

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

15 Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. 16 Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200;21:16 Kilomita 2,200 hapa ni sawa na maili 1,200. urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 17 Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 14421:17 Dhiraa 144 ni karibu mita 65. kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    15 Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. 16 Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama stadioni 12,00021:16 ni kama kilomita 2,200; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 17 Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa mia moja na arobaini na nne (144)21:17 ni karibu mita sitini na tano kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    15 Eze 40:3,5Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Eze 43:16;48:16,17Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu moja na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia moja na arubaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, ambacho malaika alitumia.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.