Kitabu Na Mwana-Kondoo
1 Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nje, kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba. 2 Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, akisema, "Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua kitabu?"