Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 12:2,5,12-16

2 Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga.

5 Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii.

12 Mara Petro alipotambua hili alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana aliyeitwa pia Marko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 13 Petro alipobisha hodi kwenye lango la nje, mtumishi wa kike jina lake Roda, akaja kumfungulia. 14 Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi mno akarudi bila kufungua na kuwaeleza kwamba, "Petro yuko langoni!"

15 Wakamwambia yule mtumishi wa kike, "Umerukwa na akili." Alipozidi kusisitiza kuwa ni kweli, wakasema, "Lazima awe ni malaika wake."

16 Lakini Petro aliendelea kugonga langoni, nao walipofungua lango na kumwona Petro, walistaajabu sana.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.