Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 19:18-20

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

18 Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu. 19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma 50,00019:19 Drakma ilikuwa ni sarafu ya fedha, thamani yake ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja. za fedha. 20 Hivyo neno la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    18 Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu. 19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma elfu hamsini19:19 Drakma moja ilikuwa na thamani sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja. za fedha. 20 Hivyo neno la Bwana Isa likaenea sana na kuwa na nguvu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. 19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha elfu hamsini.19:19 Yapata kama shilingi 34,000.20 Mdo 6:7;12:24Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.