Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 2:42-47

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Ushirika Wa Waumini

42 Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Walioamini wote walikuwa mahali pamoja, nao walikuwa na kila kitu shirika. 45 Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa wale waliokuwa wakiokolewa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    42 Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Waumini wote walikuwa mahali pamoja, nao wakashirikiana katika mambo yote. 45 Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu2:46 Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu., wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    42 Mdo 20:7Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

    43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Mdo 4:32-35Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote kishirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja. 46 Mdo 2:42Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 Mdo 4:4;5:14;11:21;14:1wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.