28 Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. 29 Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi. 30 Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate.
Matendo Ya Mitume 20:28-30
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
28 Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho wa Mungu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Chungeni jumuiya ya waumini ya Mungu, aliowanunua kwa damu yake mwenyewe. 29 Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa-mwitu wakali watakuja kati yenu, ambao hawatalihurumia kundi. 30 Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate.
- SRUV Swahili Revised Union Version
28 Zab 74:2;1 Tim 4:16;1 Pet 5:2Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. 29 Mt 7:15;10:16;Yn 10:12Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; 30 1 Yoh 2:19;Gal 4:17tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawafuatie wao.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.