Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 25:10-12

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

10 Paulo akasema, "Mimi sasa nimesimama mbele ya mahakama ya Kaisari, ambako ndiko ninakostahili kushtakiwa. Kama vile wewe mwenyewe ujuavyo vyema kabisa sijawatendea Wayahudi kosa lolote. 11 Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!"

12 Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, "Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utakwenda!"

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    10 Paulo akasema, "Mimi sasa nimesimama mbele ya mahakama ya Kaisari, ambako ninastahili kushtakiwa. Kama vile wewe mwenyewe unavyojua vyema kabisa sijawatendea Wayahudi kosa lolote. 11 Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!"

    12 Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, "Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utaenda!"

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    10 Paulo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, ndipo panipasapo kuhukumiwa; sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana. 11 Basi ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari. 12 Basi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufani kwa Kaisari! Basi, utakwenda kwa Kaisari.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.