Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 3:6-8

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

6 Ndipo Petro akamwambia, "Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!" 7 Petro akamshika yule mtu kwa mkono wa kuume akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. 8 Akaruka juu na kusimama, akaanza kutembea. Kisha akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akitembea na kurukaruka na kumsifu Mungu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    6 Ndipo Petro akamwambia, "Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nitakachokupa. Kwa jina la Isa Al-Masihi wa Nasiri, tembea!" 7 Petro akamshika yule mtu kwa mkono wa kuume akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. 8 Akaruka juu na kusimama, akaanza kutembea. Kisha akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akitembea na kurukaruka na kumsifu Mungu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    6 Mdo 3:16Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. 7 Akamshika mkono wa kulia, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. 8 Yn 5:14Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akirukaruka, na kumsifu Mungu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.