36 Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamuuliza Filipo, "Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?" [ 37 Filipo akamwambia, "Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa." Akajibu, "Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu."] 38 Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Wakateremka kwenye maji wote wawili, yule towashi na Filipo, naye Filipo akambatiza.
Publicidade
Publicidade