Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 9:1-5,15,17,20

Kuokoka Kwa Sauli

1 Wakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. 3 Basi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, "Sauli, Sauli, mbona unanitesa?"

5 Sauli akajibu, "U nani wewe, Bwana?"

Ile sauti ikajibu, "Mimi ni Yesu unayemtesa.

15 Lakini Bwana akamwambia Anania, "Nenda! Mtu huyu ni chombo changu kiteule nilichokichagua, apate kulichukua Jina langu kwa watu wa Mataifa na wafalme wao na mbele ya watu wa Israeli.

17 Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, "Ndugu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu."

Sauli Ahubiri Dameski

20 Papo hapo akaanza kuhubiri kwenye masinagogi kwamba "Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu"

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.