Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo Ya Mitume 9:1-9

Kuokoka Kwa Sauli

1 Wakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. 3 Basi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, "Sauli, Sauli, mbona unanitesa?"

5 Sauli akajibu, "U nani wewe, Bwana?"

Ile sauti ikajibu, "Mimi ni Yesu unayemtesa. 6 Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda."

7 Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila kuwa na la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8 Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. 9 Naye kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu naye hakula wala kunywa chochote.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.