3 Basi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, "Sauli, Sauli, mbona unanitesa?"
5 Sauli akajibu, "U nani wewe, Bwana?"
Ile sauti ikajibu, "Mimi ni Yesu unayemtesa. 6 Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda."
7 Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila kuwa na la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8 Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. 9 Naye kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu naye hakula wala kunywa chochote.