Pular para o conteúdo
Publicidade

Danieli 7:9-11

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

9 "Nilipoendelea kutazama,

"viti vya enzi vikawekwa,

naye Mzee wa Siku akaketi.

Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;

nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.

Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto,

nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.

10 Mto wa moto ulikuwa unatiririka,

ukipita mbele yake.

Maelfu elfu wakamhudumia;

kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake.

Mahakama ikakaa kuhukumu,

na vitabu vikafunguliwa.

11 "Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 "Nilipoendelea kutazama,

    "viti vya utawala vikawekwa,

    naye Mzee wa Siku akaketi.

    Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;

    nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.

    Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka miali ya moto,

    nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.

    10 Mto wa moto ulikuwa unatiririka,

    ukipita mbele yake.

    Maelfu elfu wakamhudumia;

    kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake.

    Mahakama ikakaa kuhukumu,

    na vitabu vikafunguliwa.

    11 "Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia hadi yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 1 Kor 15:24;Zab 90:2;104:2-4;Ufu 20:4;1:14Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Kum 33:2;Zab 68:17;Mt 25:31,32;Ufu 5:11;20:12Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu wakamtumikia, na mamilioni wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. 11 Ufu 19:20Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nilitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.