5 Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa,
lakini wafu hawajui chochote,
hawana tuzo zaidi,
hata kumbukumbu yao imesahaulika.
6 Upendo wao, chuki yao na wivu wao
vimetoweka tangu kitambo,
kamwe hawatakuwa tena na sehemu
katika lolote linalotendeka chini ya jua.
10 Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.