11 Bwana akamwambia Mose, 12 "Nimesikia manungʼuniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ "
13 Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. 14 Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, "Hiki ni nini?" Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Mose akawaambia, "Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle.