Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 30:1,6-8,10

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

1 "Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 6 Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe.

7 "Itampasa Aroni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa. 8 Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za Bwana kwa vizazi vijavyo. 10 Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Bwana."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 "Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 6 Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la ule Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ule Ushuhuda, mahali nitakapokutana nawe.

    7 "Itampasa Haruni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa. 8 Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za Mwenyezi Mungu kwa vizazi vijavyo. 10 Mara moja kwa mwaka Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Mwenyezi Mungu."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Kut 37:25;40:5;Ufu 8:3Nawe fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita. 6 Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe. 7 Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza. 8 Na Haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Bwana katika vizazi vyenu vyote. 10 Law 23:27Naye Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka; kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote; ni takatifu sana kwa BWANA.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.