Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 31:1-6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Bezaleli Na Oholiabu

1 Ndipo Bwana akamwambia Mose, 2 "Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 4 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. 6 Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe:

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 2 "Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 4 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. 6 Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia.

    "Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe:

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Kut 35:30;1 Nya 2:20Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; 3 Kut 35:31;1 Fal 7:14;Isa 28:26;1 Kor 12:4-8nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. 6 Kut 35:34;28:3;36:1Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza;

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.