Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 8:8-10

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

8 Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kusema, "Mwombeni Bwana awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea Bwana dhabihu."

9 Mose akamwambia Farao, "Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako na watu wako ili kwamba vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu. Isipokuwa wale walio katika Mto Naili."

10 Farao akasema, "Kesho."

Mose akamjibu, "Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna yeyote kama Bwana Mungu wetu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    8 Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kusema, "Mwombeni Mwenyezi Mungu awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu."

    9 Musa akamwambia Farao, "Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako, na watu wako ili vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu, isipokuwa wale walio katika Mto Naili."

    10 Farao akasema, "Kesho."

    Musa akamjibu, "Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna yeyote kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    8 Kut 9:28;10:17;Hes 21:7;1 Fal 13:6;Mdo 8:24Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni BWANA, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee BWANA dhabihu. 9 Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu. 10 Kut 9:14;Kum 33:26;2 Sam 7:22;1 Nya 17:20;Zab 86:8;Isa 46:9;Yer 10:6,7Akamwambia, Kesho, Akasema, Na yawe kama neno lako; ili upate kujua ya kwamba hapana mwingine mfano wa BWANA, Mungu wetu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.