4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6 Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Wafilipi 4:4-7
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
4 Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini! 5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana Isa yu karibu. 6 Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.
- SRUV Swahili Revised Union Version
4 Flp 3:1;2 Kor 13:11Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. 5 Ebr 10:37;Yak 5:8,9Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu. 6 Mt 6:25-34;Kol 4:2;1 Pet 5:7;Zab 145:18;Yn 14:27Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Kol 3:15Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.