Mnara Wa Babeli
1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari11:2 Shinari ndio Babeli. nao wakaishi huko.
3 Wakasemezana wao kwa wao, "Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto." Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 4 Ndipo wakasema, "Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote."
5 Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. 6 Bwana akasema, "Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao."
8 Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.
Shemu Hadi Abramu
(1 Nyakati 1:24-27)