5 Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. 6 Bwana akasema, "Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao."
8 Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.