Kuzaliwa Kwa Isaki
1 Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 5 Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.
6 Sara akasema, "Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami." 7 Akaongeza kusema, "Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake."