6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, "Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, 8 Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: 9 Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda. 10 Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa."
15 Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. 16 Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi.
19 Yakobo akamwambia baba yake, "Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki."
24 Akamuuliza, "Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?"
Akajibu, "Mimi ndiye."
35 Lakini akasema, "Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako."
Yakobo Anakimbilia Kwa Labani
41 Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, "Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo."
43 Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani.